Mambo yanayochukizwa kuyafanya ndani ya saumu
1. Kupitisha mpaka katika kusukutuwa na kupandisha maji puani
Na hii ni kwa ajili ya kuhofia maji yasije yakaingia tumboni mwake, kwa kauli ya Mtume ﷺ: “Na fanyeni sana katika kupandisha maji puani isipokuwa wakati mtu amefunga saumu” [Imwpokewa na Abuu Daud.].2. Kumpiga busu kwa matamanio ya kimapenzi
Inachukizwa kwa aliyefunga saumu ikiwa anachelea nafsi yake kutokwa na manii au kusisimukwa kwa matamanio ya kimapenzi.Na ni juu ya aliyefunga kujiepusha na kila ambalo kwamba litampelekea kusisimukwa na kuleta harakati za kuibuka matamanio ya kimapenzi, na ikiwa anaamini nafsi yake kwamba haitompelekea katika hisia za matamanio ya kimapenzi basi hakuna kosa kwake kum’busu mkewe au mke kumbusu mumewe; kutoka kwa A’isha anasema: “Alikuwa Mtume ﷺ akipiga busu na kubashiriana ( yaani akimshikashika mkewe), na alikuwa ni m’bora zaidi kuliko nyinyi katika kumiliki matamanio ya kimapenzi [ Irbihi: Haja yake.]” [Imwpokewa na Bukharin a Muslim.].
Na kwa ajili hii inachukizwa kubashiriana kimapenzi kwa kijana kinyume na mzee kwa kuwa kijana damu yake ni moto zaidi, kutoka kwa Abu Hureirah anasema: “Kwamba kuna mtu mmoja alimuuliza Mtume ﷺ kuhusu kubashiriana mke na mume kwa aliyefunga, Mtume akampa ruhusa ya kufanya hivyo, na akaja mwengine akauliza (swali hilo hilo), Mtume akamkataza, kwani yule aliyempa ruhusa alikuwa ni mzee, na yule aliyemkataza alikuwa ni kijana” [ Imwpokewa na Abuu Daud.].
Mambo yanayoharibu Saumu
1. Kula na kunywa kwa kukusudia ndani ya mchana wa Ramadhani
Kwa kauli ya Mwenyezi Mungu U: {Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni saumu mpaka usiku} (Al-Baqarah – Aya 187).Kula kwasababu ya kazi Yoyote anayefanya kazi mahali pa mapishi ya mikate hivi na mahali pa kazi ngumungumu sio ruhusa kwao kutofunga (yaani hawafai kula mchana wa Ramadhani); kwasababu wamelazimika kama watu wengine kufunga Ramadhani.
- Maelezo
- Atakaye kula au kunywa kwa kusahau basi saumu yake imeswihi (iko sawa haina tatizo lolote), na inamlazimu kujizuia na vitu vinavyoharibu saumu pindi anapokumbuka; kwa kauli ya Mtume ﷺ: “Aliyesahau hali ya kuwa amefunga akala na kunywa, basi akamilishe saumu yake, kwani Mwenyezi Mungu amemlisha na kumnywesha (mtu huyo)” [Imwpokewa na Muslim.].
- Kinaharibu saumu chochote kile kinachoingia tumboni kwa njia ya mdomoni au puani, na chochote kinachofahamika kuwa chakula au kinywaji, kama vile sindano za lishe/chakula. Ama sindano ambazo si za chakula, kama penicillin na mfano wake, hazifunguzi saumu, kwasababu sio chakula wala kinywaji, wala sio kwa maana ya chakula.
- Chochote kinachoingizwa mdomoni kwa ajili ya kutizama kitu na vipuliza hewa vya kutibu pumu na mfano kama huu, hakiharibu saumu.
- Wanja, na matone ya kitu majimaji kutonezwa kwenye jicho na sikio na mfano wa hivi viwili havivunji saumu, kwasababu hakuna dalili ya vitu hivi kuharibu saumu, na kwasababu jicho sio sehemu inayotegemewa kwa kuingilia chakula na kinywaji, na vile vile matone ya kitu majimaji kwenye sikio na puani, lakini ubora kwa haya matone ni kujitenga nayo, kwa jinsi alivyokataza Mtume ﷺ kuhusu kupita mpaka katika kupandisha maji puani kwa aliyefunga, [Imwpokewa na Tirmidhi.] na kwasababu ni sehemu inayopitisha chakula hadi tumboni.
- Anapotumia mtu kitu ambacho hakiliwi au kinadhuru, kama vile sigara basi atakuwa amefungua, kwasababu amekitumia kupitia sehemu inayotumika kwa chakula, nayo ni mdomo, kama nayo itakavyofahamika kuwa chakula ama kinywaji.
- Hakiharibu saumu kitu ambacho kwamba huwezi kukiepuka, kama vile vumbi la njiani, na mabaki ya chakula yaliosalia kati ya meno.
Dawa inayotumika kama chakula inaharibu saumu.
Sindano ya penicillin haiharibu saumu.(Hii ni sindano ya kukinga au kutibu madhara yanayosababishwa na bacteria).
Vipuliza hewa vya kutibu pumu haviharibu saumu.
Wanja haiharibu saumu.
Sigara zinaharibu saumu.
Mabaki ya chakula yaani katika meno hayaharibu saumu.
- Atakaye kula au kunywa kwa kusahau basi saumu yake imeswihi (iko sawa haina tatizo lolote), na inamlazimu kujizuia na vitu vinavyoharibu saumu pindi anapokumbuka; kwa kauli ya Mtume ﷺ: “Aliyesahau hali ya kuwa amefunga akala na kunywa, basi akamilishe saumu yake, kwani Mwenyezi Mungu amemlisha na kumnywesha (mtu huyo)” [Imwpokewa na Muslim.].
- Kinaharibu saumu chochote kile kinachoingia tumboni kwa njia ya mdomoni au puani, na chochote kinachofahamika kuwa chakula au kinywaji, kama vile sindano za lishe/chakula. Ama sindano ambazo si za chakula, kama penicillin na mfano wake, hazifunguzi saumu, kwasababu sio chakula wala kinywaji, wala sio kwa maana ya chakula.
- Chochote kinachoingizwa mdomoni kwa ajili ya kutizama kitu na vipuliza hewa vya kutibu pumu na mfano kama huu, hakiharibu saumu.
- Wanja, na matone ya kitu majimaji kutonezwa kwenye jicho na sikio na mfano wa hivi viwili havivunji saumu, kwasababu hakuna dalili ya vitu hivi kuharibu saumu, na kwasababu jicho sio sehemu inayotegemewa kwa kuingilia chakula na kinywaji, na vile vile matone ya kitu majimaji kwenye sikio na puani, lakini ubora kwa haya matone ni kujitenga nayo, kwa jinsi alivyokataza Mtume ﷺ kuhusu kupita mpaka katika kupandisha maji puani kwa aliyefunga, [Imwpokewa na Tirmidhi.] na kwasababu ni sehemu inayopitisha chakula hadi tumboni.
- Anapotumia mtu kitu ambacho hakiliwi au kinadhuru, kama vile sigara basi atakuwa amefungua, kwasababu amekitumia kupitia sehemu inayotumika kwa chakula, nayo ni mdomo, kama nayo itakavyofahamika kuwa chakula ama kinywaji.
- Hakiharibu saumu kitu ambacho kwamba huwezi kukiepuka, kama vile vumbi la njiani, na mabaki ya chakula yaliosalia kati ya meno.
2. Kufanya Tendo la Ndoa
Kwa kauli ya Mwenyezi Mungu U { Mmehalalishiwa usiku wa saumu kuingiliana na wake zenu} (Al-Baqarah – Aya 187).Na “Ar-Rafath” ni neno la kiarabu lililotumika katika Aya hii kumaanisha kuingiliana – yaani kufanya tendo la ndoa, basi yoyote atakaye ingiliana na mkewe au mumewe hali ya kuwa amefunga, saumu yake itakuwa imeharibika, na atalazimika ailipe siku hiyo, na pamoja na kuilipa ni juu yake kutoa kafara nzito, nayo ni kuacha huru mtumwa, akiwa hatopata mtumwa wa kumuacha huru, atalazimika kufunga miezi miwili mfululizo, na akiwa hawezi kufunga atalazimika kulisha masikini sitini, kama ilivyothibiti kutoka kwa Abu Hureiah t Anasema: “ Alikuja mtu mmoja kwa Mtume ﷺ akasema nimeangamia. Mtume akamuuliza: Una nini? Akajibu: Nimemuingilia mkewangu ndani ya Ramadhani. Mtume akamuuliza: Waweza kuacha mtumwa huru?. Akajibu: Siwezi.. Mtume akamuuliza: je waweza kufunga miezi miwli mfululizo? Akasema: Siwezi. Mtume akamuuliza: Basi waweza kulisha masikini sitini?. Akasema: Siwezi. Mtume akamwambia: Kaa. Akakaa. Mtume ﷺ akaleta chombo ambacho ndani yake mna tende. Akasema: Chukua (hiki chombo) wende ukatolee sadaka. Akasema yule mtu: Je kuna fakiri zaidi yetu? (yaani maskini kuliko familia yake). Mtume akacheka mpaka yakaonekana magego ya meno yake, akasema: Lisha familia yako ( hizo tende)” [Imwpokewa na Bukharin a Muslim.].
Na inakuwa kafara inafuata mfumo huu, hivyo basi mtu asilishe maskini isipokuwa akiwa hawezi kufunga hiyo miezi miwili mfululizo, wala asifunge isipokuwa ikiwa hawezi kuacha huru mtumwa.
Na inamlazimu mwanamke kutoa kafara ikiwa ameridhiana na mumewe kufanya tendo la ndoa, na iwapo amelazimishwa na mumewe kuingiliana basi saumu yake imeharibika na itamlazimu mwanamke huyo kuilipa saumu hiyo peke yake bila ya kutoa kafara.
Na ni katika maana ya jimai (tendo la ndoa) kujitoa manii kwa kukusudia, Mtu akitokwa na manii kwa kubusiana, au kwa kugusa au kwa kutumia mkono, basi saumu yake itaharibika, kwa sababu hiyo ni katika shahawa inao haribu saumu, na itakuwa ni juu yake kuilipa saumu yake wala hatolazimika kutoa kafara, kwa sababu kafara imekuja kwa tendo la ndoa peke yake.
Mtu akibusu au akigusa au akifikiria akatokwa na madhii saumu yake ni swahihi. kwa kutokuwa na dadili yakuharibu saumu kwa kutokwa na madhi
Mtu anapo lala akaota, au akatokwa na manii bila ya shahawa kama kuwa mgonjwa, saumu yake ni swahihi kwa sababu hayakutoka kwa hiyari yake.
Mtu anapo amka na janaba la tendo la ndoa kabla ya alfajiri au akaota, saumu yake ni swahihi na ni juu yake kuoga ili apate kuswali alfajiri na jamaa, imethubutu kutoka kwa bibi A’isha t Kwamba Mtume ﷺ Alikuwa akiingiliwa na Alfajiri na yeye akiwa na janaba la mkewe, kisha akioga na akifunga
3. kujitapisha kwa kusudi
Nao ni mtu kutoa kilichoko tumboni kutokana na chakula au kinywaji kwa njia ya mdomo kwa kusudi, ama akishindwa na akatoka bila ya khiyari yake haiathiri saumu yake kwa neno lake Mtume ﷺ ( Mwenye kushindwa na matapishi basi hana haja ya kukidhi na mwenye kujitapisha kwa kusudi basi alipe)4. Damu ya Heidhi na Nifasi
Wakati wowote mwanamke atakapo ona damu ya hedhi au nifasi japo kuwa ni wakati wa jioni kabla ya kutwa jua kwa mda mchache saumu yake itaharibika na atawajibika kuilipaFaida
- Kauli yenye nguvu ni kuwa kuumika hakuvundi saumu kwa sababu Mtume ﷺ Aliumika na hali yakuwa amefunga, Amepokewa kutoka kwa said Al’khudriy t akisema (Aliruhusu Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ Kubusu kwa aliyefunga na kuumika, lakini inachukizwa kuumika kwa ajili ya kudhofika, Aliulizwa Anas bin Maalik t Mulikuwa mukichukiza kuumika kwa alie funga? Akasema la ila kwa ajili ya kudhofika.- Haidhuru mtu kutokwa na damu katika jaraha, au kung’oa jino au kutokwa na damu za puwa, au kutoa damu kwa ajili ya kujipma, au kujitolea, yote haya hayaharibu saumu.
No comments