| simulizi | ndoa yangu 40&41&42

Share:
Taratibu nilianza kusukuma stuli
nilioikanyaga ili idondoke na nijinyonge,
Muomba kifo hakosi basi stuli ilidondoka
kamba ikaninyonga.
“Ahiiiii”nilitoa sauti moja kwa shida
sana.Kutoa neno la zaidi,nilijijigeuza na
nikawa natapatapa kama mfa maji.
“Haraka Getu aliamka na kuekekea sauti
ilipotoka, aliamini nilikuwa nianajiua akajuta
na kujilaumu kwanini alinipa maneno ya
ukali badala ya kunifariji.
“Dhambi zote ni mimi, isingekuwa mimi
asingejiua, yanipasa nijitahidi kumnusuru na
kifo,” Getu alianza kuniita kwa sauti ya
huruma, “Sweedy…Sweedy… naomba
unisikilize mkeo naongea. Niwie radhi
nilikuwa na kutania nimekubali kuwa na
rafiki yako. Naomba unielewe mpenzi
nitalitunza penzi lako na siri yako. Kama
nikujiua basi nisubiri tuongee nitakuacha
uendelee kujiua.” Getu aliendelea kuniita
bila ya kupata kujibiwa. Kilikuwa kitendo
cha haraka alichukua uamuzi wa kuvunja
mlango na kuingia ndani, alinikuta nikiwa
nimeningia mapovu ya kitoka puani.Aliona
kisu kilichokuwa
mezani,Hakupendakupoteza muda ,kwa
mwendo wa umeme alikata kamba na
nikadondoka chini kama gunia la maharage,
aliponigusa alipeleka mkono kifuani kuona
kama nilikuwa hai. Ajabu ni kwamba
hakusikia mapigo ya moyo ya kienda. Miguu
ndio ilikuwa nikiitupatupa huku na kule,
ulimi ukiwa nje kama wa kenge. Hali
iliyomfanya asijidanganye kuwepo hai tena
na kuamini zisingepita dakika kumi
ningepoteza uhai.
Uzito wangu haukuwa kigezo kikubwa cha
kumfanya Getruda ashindwe kunibeba,
alijitahidi alivyo weza kunitoa nje ambako
alipiga simu kwa dereva teksi aliyemfahamu.
Dakika takribani mbili ,alisikia gari
likiegeshwa nje ya jengo letu.
“Vipi shem. Imekuwa je?”Dereva teksi
aliuliza.
“Wee achatu.Hebu tumuwahishe hospitali
mazungumzo baadaye”
Walinibeba juu juu hadi kwenye gari, dereva
akafungua mlango wa nyuma ambako
walinilaza chali na kufunga
mlango.Hawakukawia kufika hospitali ya
rufaa Mount meru kwa matibabu
zaidi.Getruda aliniingiza ofisi ya dakitari wa
zamu.
“Anasumbuliwa hasa na nini?” “Amevamiwa na majambazi ambao
walimnyonga kwa kutumia kamba”Getruda
alidanganya wazi wazi.Huku akiuma mdomo
wa chini kana kwamba alijawa na dhahabu
kali.
“Sasa umeripoti polisi?”
“Daktari mbona unaniuliza maswali ya sio na
msingi kabisa.Wewe unataka ripoti ama
kumtibu mgonjwa?”
“Hatuwezi kutibu bila kupokea karatasi ya
PF3 kutoka polisi”
“Dokta kipi bora .Kuokoa maisha ya mgonjwa
ama kumwacha afe kwa sababu ya PF3?”
“Kuokoa maisha yake”Dokta akajibu
akichukua vipimo vyake.
“Basi kumbe unajua. PF3 baadae, nisamehe
kama nimekuudhi”Getruda alimwomba radhi
Dokta.
Dokta alinishughulikia kwa haraka.Nilitibiwa
kwa makini na baada ya saa nzima nilipata
ahuen.Ila kooni nilihisi maumivu kwa ndani.
**********
Zikawa zimepita Siku mbili toka
nilipookolewa na Mke wangu,Getruda pale
nilipokuwa najiua kifo cha taabu.
“Mume wangu nilikuwa nikikutania .
Tafadhali usijaribu kujiua tena. Nimekubali
mlete huyo rafiki yako leo nimuone kama
sura yake ina tapisha au laa!” Getruda
hakupenda kufanya hivyo aliamua kukubali
ili kuninusuru kifo. Sauti ya Getruda
ilipenyeza kwenye ngoma ya masikio yangu
fundo kali la sononeko liliingia
moyoni.Nikajivuia kulia kwa nguvu zote
lakini nilijikuta machozi yakichuruzika
taratibu bila kujua.
“Sawa mke wangu utamuona nitakapomleta
jioni,” Ilikuwa asubuhi na mapema, majira ya
saa moja na nusu.
“Mmmm! Lakini Getruda
unanipenda.Isingekuwa wewe basi nilikuwa
mfu”Nilimweleza Getruda.
“Kumbe unalijua.Mkojo ulishaanza kukutoka”
“Masihara hayo.Inamaana nilikikojolea kama
mtoto”
“Ndio”Getruda alinijibu akainuka kitini na
kuelekea kwenye jokofu ambako alilifungua
na kunipatia Juisi baridi ya machungwa.
“Karibu mpenzi”
“Ahsante mpenzi”Niliipokea na kumtolea
tabasamu,lakini nilipokumbuka kwamba
nahitajika kumtambulisha bosi wangu.Moyo
ulisinyaa na kunyauka kama jani la tumbaku
lililosubiri kusagwa.“Mpenzi nataka kwenda kujipumzisha
kidogo”
“Sawa,ila usisahau kwenda kumleta rafiki
yako jioni”Nilishituka na kutulia kama
sekunde kadhaa ,kisha nikageuka kumtizama
mke wangu.
“Utaniamsha baada ya saa moja.
Ok, bye”Nilijikaza kutoa tabasamu ambalo
pengine lilionekana dhahiri la kulazimisha,
huku moyo ukiniuma kama kutu inavyokula
chuma taratibu na kukiozesha chote.
“Nije tujipumzishe wote?”Getruda alinieleza
wakati nikiwa nimempa mgongo.
“Poa. Ukipenda”Nilimjibu damu zikienda
mbio ,ungeweza kuhisi nimekimbia umbali
mrefu bila kupumzika.
Getruda alinifuata chumbani kama
alivyoomba.Nilijitupa kitandani kiuvivu
uvivu nae akajibweteka kwenye sofa moja
lililomo chumbani.Ingawa nilifumba macho
lakini sikuwa hata na lepe la usingizi,
mawazo yangu yalimezwa na taswira ya
maisha ya unyumba.Nilijiuliza bila kupata
jawabu sahihi kwamba ugonjwa huwa
niliupata wapi na nani aliyenipa?.
Nikiwa nimelala nilihisi vidole laini zikitalii
mwilini mwangu.Hata hivyo sikushituka
kwani nilihiosi alikuwa mke wangu.Vidole
hivi vilizunguka huku na kule bila
kupumua,nilihisi kama kero ama mdudu
fulani akinitembelea akini kwarua. Sikuona
raha zaidi za mateso tu.
“Hallo Sweedy”
“Na..a.amu”Nilikokoteza maneno,nikiwa
nimetulia utadhani mbwa anayetolewa kupe.
“Unanipenda?”
“Saaana tu”
“Kwanini hunipi haki yangu kama kweli
unanipenda?”
“Haki ipi?.Si una jua matatizo yangu sasa
unataka nini tena”
Nilihisi Getruda akinitibua akili
yangu.Niliinukla na kutoka nje.
“Getruda unanitesa. Tumepanga nini na
wewe unataka nini?”
Nilitulia kidogo nikaendelea, “Moyo wangu
unasononeka sana. Laiti ningelijua
nisingeoa, maisha gani haya yananitesa kiasi
hiki?”Nilijikuta nikilia ovyo kama toto jinga
lenye kudeka ovyo.Kilio changu lilikuwa
rohoni.na aliyejua alikuwa muumba
pekee.Getruda alikuja kunibembeleza kwa
hofu kwamba ningechukua maamuzi ya
kijinga tena. Aliniandalia chakula
mezani.Tulisali kisha tukala .
Saa nane mchana baada ya kupata mlo wa
mchana nilimuaga Getruda nikiwa naelekea
ofisini kumueleza Mzee Jophu yaliyosibu
katika unyumba wangu. 

No comments