
UBORA WA SWAUMU NA FADHILA ZAKE
Linalo julisha ubora na fadhila za Funga ni maneno ya Mtume (Swallah Llahu Alayh Wassalam) haya yafuatayo-: "الصوم جنة من النار كجنة أحدكم من القتال " .) 1 (Kufunga ni kinga ya Moto kama vile kinga ya mmoja wenu katika vita".(Ahmad, Nasaiy) من صام يوما في سبيل الله باعد الله بذلك اليوم حر جهنم عن وجهه سبعين خريفا . ) 2 ( Atakae funga siku moja katika njia ya Allah, Allah atamwepusha kwa utukufu wa siku hiyo uso wake na joto la moto wa Jahannam umbali wa miaka sabiin" (Ahmad, Nasaiy,Ibn Majah,Tirmidhi( أن في الجنة باب يقال له الريان يقال يوم القيامة أين الصائمون هل لكم إلى الريان من دخله لم يظمأ أبدا فإذا دخلوا أغلق عليهم فلم يدخل فيه أحد غيرهم " 3Hakika peponi kuna mlango unaitwa Rayyan, pata semwa siku ya Qiyama; wako wapi waliokuwa wakifunga waingie katika mlango huu? Watakapo ingia hawatohisi kiu tena na utafungwa mlango wake hatoingia humo ila aliyedumu na ibada ya Funga" (Bukhari,Muslimu,Nasaiy) Na hadithi nyinginezo. Na mlango huu umepewa jina hilo kunasibiana na sifa ya Swawm ambayo inampa mtu kiu kutokana na athari ya kufunga. Mara nyingi mtu anapofunga hatamani chakula kama anavyotamani maji .
FADHILA ZA MWEZI WA RAMADHANI
Ameeleza Mtume (Swallah Llahu Alayh Wasalam) ubora/fadhila za mwezi wa ramadhani katika hadithi zifuatazo-: الصلوات الخمس والجمعة إلى الجمعة ، ورمضان إلى رمضان مكفرات لما بينهن ، إن اجتنبت الكبائر ( ] رواه مسلم " -1 swala tano, swala ya Ijumaa hadi Ijumaa, na Ramadhani hadi Ramadhani (yote hayo) ni yenye kufuta dhambi zilizo baina yake, maadamu madhambi makubwa yataepukwa." (Muslimu) ((من صام رمضان إيماناً واحتساباً غفر له ما تقدّم من ذنبه(( ] متفق عليه " " -2 Atakaefunga Ramadhani hali ya kuamini na kutaraji thawabu atasamehewa dhambi zake zilizo tangulia" (Bukhari na Muslimu) إذا كان أول ليلة من رمضان صفدت الشياطين ومردة الجان ، وغلقت أبواب النار فلم يفتح منها باب ، وفتحت أبواب الجنة فلم يغلق منها باب ، ونادى منادٍ : يا باغي الخير أقبل ، ويا باغي الشرّ أقصر ، ولله عتقاء من النار ، وذلك كل ليلة ( " -3Inapokuwa usiku wa kwanza wa Mwezi wa ramadhani Masheitwani hufungwa na Majini wakorofi,nao hufungwa pia Milango yote ya moto,na hufunguliwa milango yote ya pepo.Hutangaza mtangazaji (malaika) kwa kusema: Ewe unaetaka kheri elekea katika kheri hiyo,na Ewe mwenye kutaka shari acha shari hiyo, Allah huwa anawaacha hu ru na moto.Na maneno haya husemwa kila usiku" (Tirmidhi(. Pia ndani ya mwezi huu ndimo Qur'an iliteremshwa kutoka ktk Lawhum Mahfuudh ilaa samaai dduniya (Kutoka LawhimMahfuudh mpaka mbingu ya kwanza. Hivyo kwa ubora wa Qur'an basi inaunyanyua mwezi huu na kuwa bora kama Allah alivyosema katika Qur'an kuwa-: "Mwezi wa Ramadhaan ni mwezi ambao imeteremshwa Quraan ili iwe uongozi kwa watu na hoja na upambanuzi (Baina ya haki na batil)” (Qur'an Baqarah:185( Kitu kingine kinachoupa ubora mwezi huu ni Usiku wa Cheo/Laylahtul qadr kwani ktk usiku huu ndimo Qur'an ilishuka na usiku huu ukafanywa kuwa bora zaidi ya miezi elfu moja. Kama Allah alivyosema-: " Huo ni usiku wa hishima ni bora kuliko miezi elfu.Huteremka Malaika na roho (za viumbe watakatifu) katika (usiku) huo kwa idhini ya Mola kwa kila jambo.Ni amani (usiku) huo mpaka mapambazuko ya alfajiri" (Qur'an 97:3-5( Yaan mtu akifanya Ibada ndani ya usiku huo basi ibada ile huandikwa/hulipwa sawa na mtu aliyefanya ibada hiyo kwa miezi elfu moja. Pia ndani ya mwezi huu Dua zetu hupokelewa kwa kila mwenye kuomba na haya tunayapata Katika hadiyth iliyopokewa na Imaam Ahmad: "Kutoka kwa Jaabir (radhiya Allaahu 'anhu) kwa isnadi iliyo nzuri kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Amesema: "Kila Muislam du'a zake ni zenye kukubaliwa atapomuomba Allah katika mwezi wa Ramadhaan". Kuna Fadhila nyingi katika mwezi huu ambazo zimeufanya mwezi huu kuwa na ubora ndani yake na ikawa ni furaha kubwa kwa Muumini kupitikiwa/kufikiwa na mwezi huu na akaudiliki huku akiwa na afya nzuri akawa ni mwenye kutekeleza Ibada zinazopatikana ndani ya mwezi huu.
UBORA WA AMALI NJEMA NDANI MWEZI WA RAMADHANI.
Thawabu za amali njema huongezwa kwa sababu nyingi miongoni mwazo ni utukufu na ubora wa zama,kama mwezi wa Ramadhani. Zifuatazo ni baadhi tu ya amali njema zinazoongezewa thawabu katika Mwezi wa Ramadhani: .1 Kusimama usiku kwa Ibada Mtume(Swallah Llahu Alayh Wassalam) kasema: من قام رمضان إيماناً واحتساباً غفر له ما تقدم من ذنبه ( ] متفق عليه [ Atakae simama Ramadhani ilhali ya kuamini na kutaraji thawabu Allah atamsamehe dhambi zake zilizo tangulia" (Bukhari na Muslimu) . 2 Kufanya Umra.Mtume(Swallah Llahu Alayh Wassalam) anasema: ) عمرة في رمضان تعدل حجة معي ( ] متفق عليه [ Umrah katika mwezi wa Ramadhani hulingana na Hijja pamoja nami" (Bukhari na Muslimu) .3Kusoma Qur-ani tukufu. Kwa kuwa Qur'an imeshushwa ndani ya mwezi huu basi kila mwenye kukithilisha kuisoma ktk mwezi huu basi anaujira mkubwa zaidi na baada ya kulitambua hilo Maswahaba walikithirisha sana kuisoma Qur'an ndani ya mwezi huu na mifano yao tunaiona hapa chini. 'Uthmaan bin 'Afaan (Radhiya Allaahu 'anhu) kila siku akisoma Qur-aan yote yaani anakhitimisha mara moja kwa siku, kwa maana, msahafu mzima anausoma kwa siku moja. Na walikuwa baadhi yao katika wema wakisoma Qur-aan yote kwa siku tatu,wengine kwa wiki moja na wengine kwa siku kumi.Walikuwa wakisoma Qur-aan ndani ya Swalah na nje ya Swalah
No comments