| MAPISHI | Wali Wa Kichina Na Mayai

Share:
Vipimo
Mchele (Basmati) - 3 vikombe
Mbogamboga za barafu
(karot, njegere, spring beans na mahindi) - 1 kikombe
Kuku  Kidari - 1 LB (ratili)
Mayai - 2 mayai
Vitunguu (vikubwa) - 2 au 3 vidogo       
Pili pili manga - 1 kijiko cha chai
Paprika - 1 kijiko cha chai
Chumvi - Kiasi
Mafuta - 1/3 kikombe cha chai
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha supu
Tangawizi - 1 kijiko cha chai    
Kidonge cha supu - 1
Soy sauce - 2 vijiko vya supu                                                            


Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kuku
Kata kidari cha kuku vipande vidogo vidogo vya kiasi. 
Tia mafuta kidogo katika wok (karai ya kichina)
Kisha mtie kuku, thomu, tangawizi, soy sauce, pilipilimanga, paprika  chumvi.
Tia mboga za barafu, kidonge cha supu, kaanga  kuku na mboga viwive yitu vyote na mchanganyiko ukauke.

Namna Ya Kutayarisha Na kupika Wali
Roweka mchele wa basmati kwa muda wa saa au zaidi.
Halafu chemsha mchele pamoja na chumvi
Wacha uchemke asilimia 70%
Chuja maji na weka kando
Katika sufuria, tia mafuta kidogo tu
Kisha tia mayai mawili ukaange haraka haraka (crumbled egg)
Changanya mchanganyiko wa kuku na mboga
Kisha tia wali changanye vizuri
Rudisha katika moto, funika upikike kidogo hadi uive
Kisha pakua katika sahani  na tolea na mayai ya kuchemsha ukipenda.

No comments