| MAPISHI | Pilau Ya Nafaka Na Nyama Ya Kusaga

Share:

MAHITAJI

Mchele  - 3 vikombe
Nyama ya kusaga -  1 LB
Mchanganyiko wa Nafaka upendazo; maharagwe, njegere, mbaazi n.k 1 mug 
Vitunguu maji  kata vipande vipande -  3 vya kiasi
Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi - 2 vijiko vya supu
Mafuta - ½ Kikombe
Mchanganyiko wa bizari (Garam Masala) - 2 vijiko vya chai
Vipande vya supu (Maggi cubes)  -  3
Maji (inategemea mchele) - 5
Chumvi  - Kiasi

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
  1. Osha mchele na roweka.
  2. Weka mafuta katika sufuria na kaanga vitunguu mpaka viwe brown.
  3. Tia Thomu na tangawizi, kaanga kidogo.
  4. Weka nyama ya kusaga, chumvi na garam masala, endelea kukaanga mpaka nyama iwive.
  5. Mwaga maji yaliomo katika kopo la nafaka na utie nafaka pekee humo.
  6. Tia maji  na  vipande vya supu (Maggi cubes) huku unavivuruga, koroga kidogo.
  7. Tia mchele, koroga kidogo.
  8. Funika na pika kwa moto mdogo mpaka karibu na kukauka ukikorogoka kidogo.  (kama unavyopika pilau ya kawaida)
  9. *Epua uipike katika moto wa oven 350-400  Deg kwa muda wa dakika  15. 
  10. *Kama sufuria uliyotumia sio ya kupikia katika oven, mimina katika chombo chochote kinachotumika kwa oven kama bakuli la  pyrex au treya za  foil.
  11. Pakua katika sahani na iko tayari kuliwa.

Post a Comment

No comments