TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

Share:
Image result for Edinson Cavani
Real Madrid huenda ikawasilisha dau la £89m ili kumnunua mshambuliaji wa PSG na Uruguay Edinson Cavani, 31, ili kuchukua mahala pake Cristiano Ronaldo, ambaye alijiunga na Juventus. (AS - in Spanish)
Manchester United wameambia Leicester City wanataka kumsaini beki wa Uingereza Harry Maguire ,25, mwenye thamani ya £65m. (Mirror)
United wamewasilisha ombi la kutaka kumsaini winga wa Eintracht Frankfurt mwenye umri wa miaka 24 Ante Rebic. (Mail)

Liverpool wamekubali mkataba wa miaka miwili na beki wa Croatia Domagoj Vida, 29, lakini atalazimika kununuliwa kwa bei ya Besikitas ya £22m . (A Spor - in Turkish)
Real Madrid imeingia katika makubaliano na kipa wa Chelsea na Ubelgiji Thibaut Courtois,26. (Mail)

Chelsea na Roma wanashindana katika kumsajili winga wa Jamaica Leon Bailey, 20, kutoka klabu ya Bayer Leverkusen. (Evening Standard)

Chelsea inachunguza kiungo wa kati wa Lazio na Serbia Sergej Milinkovic-Savic, kwa lengo la kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 . (Independent)

Mkurugenzi wa Everton Marcel Brands ameelekea Barcelona ili kuendelea na mazungumzo ya kumnunua beki wa Colombia Yerry Mina, 23, na beki wa Ufaransa Lucas Digne, 25. (Mail)
Klabu mpya ilioteuliwa kucheza ligi ya Premia Wolves pia wamewasilisha ombi la kutaka kumsaini Mina kutoka Barcelona. (Sky Sports)

Wolves imewasilisha ombi la dau la £18m ili kumsaijili winga wa Uhispania Adama Traore, 22, kutoka timu ya ligi ya mabingwa Middlesbrough. (Sun)
Crystal Palace inafanya mazungumzo ya kumsaini kiungo wa kati wa West Ham na Senegal Cheikhou Kouyate, 28, kwa dau la £10m. (Sky Sports)

Newcastle inakaribia kumsaini mshambuliaji wa klabu ya Mainz na Japan mwenye umri wa miaka 26 Yoshinori Muto. (Kicker - in German)

West Ham na Fulham zina hamu ya kumsaini beki wa kulia wa Lille na Ufaransa Kevin Malcuit, 26, kwa mkopo. (France Football - in French)
Mbingwa wa Uskochi , Celtic wana matumaini ya kumsaini kwa mkopo kiungo wa kati wa Australia kinda Daniel Arzani baada ya kukamilisha uhamisho wa kudumu katika klabu ya Manchester City kutoka klabu shirikishi Melbourne City. (Scottish Sun)
Derby County inakaribia kukamilisha usajili wa mchezaji mwenye umri wa miaka 23v ack Marriott wa Petersbrough katika makubaliano yatakayoongezeka hadi £5m. (Sky Sports)

Tetesi za soka za Jumatano
Real Madrid inajiandaa kutoa dau la £60m kumnunua mlinda lango wa Tottenham na Ufaransa Hugo Lloris, 31. (Sun)
Bilionea wa Urusi Alisher Usmanov anataka kuuza asilimia 30 ya hisa zake katika klabu ya Arsenal baada ya kukiri kwamba mmiliki mkuu wa klabu hiyo Stan Kroenke hatomwachia udhibiti wa klabu hiyo. (Financial Times)
Manchester United na Chelsea zimewasilisha ombi la kutaka kumsaini kiungo wa kati wa Bayern Munich na Uhispania Thiago Alcantara, 27, ambaye anapatikana kwa dau la £62m. (ESPN)

United pia inajiandaa kuwasaini mchezaji mbadala wa winga wa Chelsea na Brazil Willian,kupitia winga wa croatia na Eintracht FrankfurtAnte Rebic, 24. (Independent)
Tottenham na Chelsea huenda zikamnyatia winga wa Ufaransa Anthony Martial, 22, ambaye anataka kuondoka katika klabu ya Manchester United lakini kusalia katika ligi ya Premia. (Sun)

Chelsea huenda ikamkosa mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 30, huku wapinzani wao wa Serie A AC Milan wakiwa na hamu ya kumsajili raia huyo wa Argentina kwa dau la £57m. (Evening Standard)

Chelsea inakaribia kumsaini mlinda lango wa siku nyingi wa Uingereza Robert Green, 38, kama nguvu mpya kwa uhamnisho wa bure. (Sun)
Fulham imekubali makubaliano ya kumsaini mchezaji wa Ujerumani na winga wa zamani wa Chelsea Andre Schurrle, 27, kutoka Borussia Dortmund. (West London Sport)
Liverpool itamzuia mshambuliaji Daniel Sturridge, 28, msimu huu na iko tayari kumpoteza mchezaji huyo wa Uingereza msimu ujao kwa uhamisho wa bure (Liverpool Echo)

Everton na West Ham wana hamu ya kumsaini beki wa Augsburg na Austria Martin Hinteregger, 25, ambaye ana thamani ya £13m. (Sun)
Wolves wanatarajiwa kumsaini winga wa Uhispania Jonny Castro, 24, kwa mkopo wa muda mrefu kutoka knblau ya Atletico Madrid. (Mail)
Derby imeanza mazungumzo ya kutaka kumsaini mshambuliaji wa Uingereza mwenye umri wa miaka 28 Martyn Waghorn kutoka klabu mwenza ya ligi ya mabingwa Ipswich kwa dau la £8m. (Mail)
Werder Bremen imefanya uchunguzi kuhusu kumsaini kiungo wa kati wa Everton na Uholanzi , 25, Davy Klaassen. (SkySports)
Fenerbahce wamewasilisha ombi la kumsaini mshambuliaji wa Tottenham na Uholanzi Vincent Janssen, 24, ambaye alihudumu msimu uliopita kwa mkopo katika klabu hiyo ya Uturuki . (SkySports)
Celtic inapanga mazungumzo ya dharura ya kuandikisha mkataba na beki Dedryck Boyata, 27, licha ya hamu ya kumsaini raia huyo wa Ubelgiji kutoka kwa klabu za Fulham na Lyon. (Daily Record)
Mkufunzi wa zamani wa Uingereza Sven-Goran Eriksson, 70,ameanza mazungumzo ya kuchukua ukufunzi wa timu ya taifa la Iraq. (Sky Sports)

No comments