|SIMULIZI | NDOA YANGU 64&65&66
“Getruda naomba iwe siri kubwa sana.Nataka
tumuondoe Sweedy Duniani”Getruda
alishituka sana kama aliyeamshwa
usingizini. “Heee!”
“Usishituke laazizi wangu.Nimeamua hivyo
kwa manufaa yetu pia.Kila siku kujiiba iiba
,tutajiiba mpaka lini?.Heri afe tupate
uhuru….”
“Haiwezekani Jophu.Unajua dhambi ya kuua
lakini?”Getruda aliuliza.
“Acha ujinga, nani kakuambia kuna
dhambi.Nani aliyeenda akarudi akasema
kuna adhabu kali?.Niambie”
“Kwenye maandiko takatifu,maneno hayo
yapo.”Getruda alijibu akimtizama Jophu.
“Kumbe nimaandiko yaliyotungwa kama
hadithi tu.Nitajie nani alikufa akafufuka na
kutuonyeshea adhabu alizopata ahera?”
“Bwana acha mizengwe yako.Uhusiano wetu
hauwezi kuzuilika kwa sababu ya Sweedy”
“Nitakupa chochote lakini tumuue
Sweedy.Uko tayari?”Getruda alikaa
kimya,safari hii alishindwa kijibu. “Nijibu
basi?”Mzee Jophu alimhimiza.
“Nikujibu nini?”
“Kwani hujui.Sina jibu lolote.”Akamtizama
Mzee Jophu ,na kuvutakumbukumbu ya siku
ya kwanza tulipokuwa kanisani,alikumbuka
maneno mengi ya mchungaji.Akanikumbuka
nilipompiga busu la kwanza nikiwa
namvisha pete ya ndoa.Pia akakumbuka
maneno ya mama yake akimweleza juu ya
unyumba wetu.Machozi yakamtiririka
mashavuni bila kujijua.Akapandisha mkono
wa kuume ulioshika leso na kujifuta. Mzee
Jophu alinyoosha mkono na kumpatia funguo
Getruda.
“Kuanzia dakika hii.Land cruiser iliyoko nje
ni mali yako.”Getruda alishangaa hakuamini
kile alichokuwa akikiona wakati huo.
“Mpenzi ni kweli ama ni mipombe
inakusumbua akili?”
“Sijalewa wa moyo.Ninachohitaji sasa hivi, ni
kutoa uhai wa huyu hanithi”Akatulia kama
nukta tano hivi ,kisha akasema,“Sawa sawa, “Sawa”Getruda alijibu mapigo ya moyo
yakimwenda mbio.Alifikiri na kuona kwanza
alishachoka kukodi teksi kila siku.Naye
alitaka kutembelea gari la kifahari.Alitamani
akawatambishie mabinti wenziye aliosoma
nao pale Mkuu Rombo.Watajuaje kwamba
naye nitajiri pasipo kutembea na gari la
kifahari?.Aliamini mtu akiwa na pesa
huheshimika kuliko hata kitu chochote
duniani.Akajikuta moyo ukipamba na furaha
kali, “Acha afe bwana kwani nini bwana.
Mtu kama furushi la nguo, heri afe , wangapi
wameuawa na kuwaacha wake zao na
mapesa kibao.Mungu nisamehe”aliwaza
akilini.
Waliendelea kunywa na kula nyama choma
pale.Getruda alimaliza bia yake na
kuongezwa zingine mbili,tayari ubongo
ukafa ganzi.Alianza kuongea sana,tena bila
kujali kwamba alisikiwa na watu. “Mpenzi
wangu nasema hivi…nitamuua kwa mikono
yangu mwenyewe.Haina haja ya kuishi
wakati hana sifa ya kumfanya hai. Eti mume,
mume gani bwege kilasiku hapandi
kitandani mpaka nishikwe na usingizi ndio
nae apande!!!!”
“Hatakama ingelikuwa mimi.Ningetumia
akili hiyo hiyo.Unafikiri ni kazi ndogo hiyo…
fedheha bwana!”
Mzee Jophu na Getruda alikunjwa na
kuondoka zao.Walielekea nyumba moja ya
wageni ambako waliingiza gari la Gertuda na
kujipumzisha.
**************
Katika maisha yangu nina kijitabia fulani
cha kutotoka siku za mwisho wa
wiki,isipokuwa jioni tena nikiwa na mke
wangu ,Getruda. Huwa natoka katika
matembezi mafupi na kurudi nyumbani.Juma
pili hii ilikuwa ngumu kwangu.Kwanza mke
wangu hakuwepo,usishangae nikimuita mke
wangu japo sikufanikiwa kufanya tendo la
ndoa.Ni mke wangu kwa sababu nimefunga
ndoa kanisani.
Mawazo bado yalinizonga sana
akilini,niliwaza safari ya ghafla ya mke
wangu.Nilitamani sana nijue maendeleo ya
wazazi wake huko mkuu Rombo.Kingine ni
tatizo linaloniletea utata ndani ya ndoa
yangu.Nilizidi kuwaza ,kwanini ugonjwa huo
uwe kwangu tu.Kwanini usiwe kwa
fulani?.Nilitamani kunywa bia lakini lakini
nikaona si kutatua tatizo zaidi ya kuliongeza.
Nikiwa kwenye dimbi la mawazo,nilisikia
simu ikiita,nilishituka sana.Kwa haraka
nikaiendea simu ambayo niliiacha Varandani
juu ya meza.Nilifikiri mambo mengi ,nikahisi
aliyepiga simu alikuwa mke wangu akinipa
habari za mama yake,nilitegemea kupata
habari mbaya kutokana na maneno
aliyoniacha nayo Getruda jana alipokurupuka
akionekana wazi kuchanganywa na hali ya
mama yake.Nilipofika nikaiokota simu upesi
na kuipokea , “Hallo mume
wangu.Umzima ?”
“Ndio.Vipi kuhusu hali ya
mama.Anaendeleaje?”Nilimwuliza.
“Kidogo amepata ahueni.Kuna uvimbe gotini
unamsumbua”
“Utakuja lini?”
“Aaa kesho jioni.Namsaidia kumuuguza
hospitalini”
“Sawa.Nimebaki mwenyewe kama mkiwa”
“Usijali mpenzi.Upo nyumbani, na hutoki
leo?”
“Ndio,nipo sitoki bila wewe.Kwanza najisikia
vibaya kabisa sijui ni kwanini mpenzi”
“Pole sana mume wangu,ahsante mke wangu ila nakumiss saana tena saana nataman ungekuwa karibu uniliwaze kwa maneno matamu, getruda alicheka na kusema usijal mme wangu mie ni wako mama akipata nafuu nitakuja na kukubembeleza muda wote. Bhasi getruda aliniaga na kukata simu, kiukwel kila nilipokuwa nikiongea na getruda sauti yake ilikuwa ikinikosha haswa na kunifanya nitaman uwepo wake lakin kila nilipokumbuka tatizo langu machozi yalikuwa yakinitoka. Lakini Gafla nilisikia simu yangu ikiita nilipotizama ilikuwa mamba mpya na nilipopokea nikasikia Sauti ya laini ambayo ilikuwa sio ngeni katika masikio yangu ikitaja jina langu na kusema amenimiss saana na tiari ameingia Tanzania anahitaji kuonana nami nikampokee ametua uwanja wa ndege wa Kilimanjaro international airport na atahitaji kufikia hotel ya Mount meru hotel. Nikiwa bado najiuliza ni nani Huyu Mara simu yake ikakatika na kila nilipojaribu kupiga ikawa haipatikani. Nikaanza kuwaza saana atakuwa ni nani huyu au mteja wangu katika biashara ameamua kufwata bidhaa zetu kabisa nchini au atakuwa nani?
#itaendeleaaa
No comments