KISA CHA MUSA(A.S) NA HIDHIRI
SEHEMU YA 04
.....Musa kisiasa kwamba miujiza ya Musa ingewateka sio tu watu wake wa karibu bali hata wananchi wa kawaida pia. Ndio sababu akakwepa kuita miujiza na badala yake akaiita uchawi na akamwita Musa mchawi stadi (26:34). Kauli hizo zililenga kuwapotosha watu ili waone kuwa mbona hata watu wengine wanaweza kufanya uchawi. Kwa hiyo Musa aonekane mchawi tu kama wachawi wengine.
Mbali na propaganda hiyo, Firauni alieneza propaganda kwa wananchi kuwa Musa amewakejeli wazee wao wa zamani kuwa walikuwa wapotevu na walistahili kuangamizwa. Hivyo wajihadhari naye, sio Mtume bali ni mchawi anayetaka kutumia uchawi wake kukutoeni nchini mwenu. Anataka wana wa Israeili wanyakue tena madaraka kama ilivyokuwa wakati wa Yusuf. Sasa lengo la Firauni na washirika wake lilikuwa ni kuwakusanya wananchi wote nchini ili waone ule uwezo wa wachawi wakubwa ambao alitaraji ungevuruga shabaha ya Musa. Firauni aliamini kuwa mara wale wachawi watakapoyazuga macho ya watazamaji yaone fimbo zao kuwa ni nyoka, athari za muujiza wa Musa zingefutika vichwani mwa watu.
Ni kwa sababu hiyo, walikubaliana na Musa kuwa mpambano huo ufanyike siku ya sikukuu ili
watu kutoka sehemu mbalimbali washuhudie.
Na ufanyike mahala pa wazi, asubuhi kweupe ili watazamaji waone vizuri. Kutokana na uzito na umuhimu wa pambano hilo, Firauni alitoa ahadi nono kwa wachawi wake kwamba wangepata cheo cha kuwa karibu naye (7:114).
Firauni na washirika wake wakaliona pambano hilo kama karata yao muhimu ya kumshinda Musa ili kunusuru madaraka yao, hivyo watu wakahamasishwa mno kuhudhuria pambano hilo.
Walitangaziwa propaganda kuwa Musa "anataka kuwatoa katika nchi yao" (20:57). Pili "anataka kuvuruga mfumo wao wa maisha na kuleta matata katika nchi". (40:26). Tatu mchawi anayetaka kundoa sera zao zilizokuwa bora kabisa (20:63).
Kwa hiyo basi, nusura ya dini yao na nchi yao ilitegemea nguvu za wachawi wao. Yaani nchi yao pamoja na utaratibu wao wa maisha vitasalimika iwapo tu upande wao utashinda. Hiyo ni kusema kuwa kama Musa akishinda na watawala kupoteza madaraka yao ndio basi tena mfumo wa maisha utabadilishwa na kwa ajili hiyo, utamaduni wao, sanaa zao, ustaarabu wao na vizazi vyao vyote vitaangamia. Kwa ujumla propaganda zote hizo zililenga kuwashawishi watu waiunge mkono serikali katika mapano ayo.
Majibizano baina ya Musa na Firauni, tena baina ya Musa a.s. na wachawi, na hali ya Musa ya kuogopa kushindwa mbele ya wachawi, na fimbo yake ilipo zimeza kamba zao, na tena mwisho vipi yalivyo ishia mambo ya wachawi na kuamini kwao, na Firauni kuwaadhibu. Kisha ikatajwa vipi Musa alivyo toka yeye na Wana wa Israili kutokana na Firauni,musa alikimbia na wana wa islaer mpaka wakafika pwani ya bahari wana wa israeli awaoni njia nyingine wamwambia musa kwani umetuleta uku wakati akuna njia?musa akawambia tamkeni maneno ya kisha akawafundisha dua, au fimbo yake kuichapa kwenya maji bahari ilipasuka katikati na ikahacha njia musa na watu wake wakavuka na vipi alivyo zama Firauni, naye alikuwa kawafuatia baada ya kupasuka bahari kufika katikati bahari ikarejea ali yake yake ya kawaida na firauni akawa mwenye kuangamia.
vipi Musa aliokoka akafika Jabal T'ur akawaacha watu wake ili ende kwenye mlima kuzungumza na Mola wake Mlezi.
Watu wake walilia njaa nakisha musa akaomba kwa mola mlezi chukula kutoka peponi na chakula kipatikan
Na Msamaria akawafitini kwa kuwachochea waliabudu sanamu la ndama lililo undwa kwa dhahabu. Na ilikuwa ukipita upepo ndani yake hutoa sauti. Musa alikasirika kwayaliyo tokea, akamkamata kichwa nduguye akimvutia kwake.
Kisha katika Sura hii tukufu yakatokea yaliyo msibu Msamaria. Mwenyezi Mungu Subhanahu amesimulia hadithi ya kuvuka katika hadithi za Musa nanyinginezo. Na mwisho wa Sura pana mausio mema juu ya Subira, na Usamehevu, na Sala. Kisha ikabainishwa kubwatika washirikina katika matakwayao ya muujiza mwengine usio huu wa Qur'ani; na Subhanahu ameashiria hikima ya kuwatuma Mitume. Tena Sura hii tukufu imekhitimisha kwa kuashiria adhabu watakayo pata makafiri, na malipo mema watakayo pata Waumini.
Kisha katika Sura hii tukufu yakatokea yaliyo msibu Msamaria. Mwenyezi Mungu Subhanahu amesimulia hadithi ya kuvuka katika hadithi za Musa nanyinginezo. Na mwisho wa Sura pana mausio mema juu ya Subira, na Usamehevu, na Sala. Kisha ikabainishwa kubwatika washirikina katika matakwayao ya muujiza mwengine usio huu wa Qur'ani; na Subhanahu ameashiria hikima ya kuwatuma Mitume. Tena Sura hii tukufu imekhitimisha kwa kuashiria adhabu watakayo pata makafiri, na malipo mema watakayo pata Waumini.
Kuna wakati nabii Musa (‘Alayhi Ssalaam) alimuuliza Allah (Sub-haanahu wa-ta’aala): “Ewe Allah, Umenitunuku heshima maalum ya kuongea Nawe moja kwa moja. Je, kuna yeyote mwingine uliyempa heshima hii?” Allah Alimjibu: “Ewe Musa, katika zama za mwisho kutakuwa na umma, nao utakuwa ni umma wa Muhammad (Swalla-llahu ‘alayhi wasallam) watakaokuwa na midomo na ndimi zilizokauka, miili iliyodhoofu, macho yaliyozama, maini makavu, na matumbo yenye njaa --- wao wataniita (ktk du’a zao) Nami nitakuwa karibu yao mno kuliko Nilivyo kwako. Ewe Musa, unavyoongea nami, kuna vizuizi 70,000 baina yako na Yangu, lkn hakutakuwa na kizuizi baina Yangu na umma wa Muhammad (SAW) wakati wanapofuturu. Ewe Musa, Nimejitwisha dhamana kuwa Sitaikataa du’a ya mwenye kufunga wakati wa anapofuturu!”
ITAENDELEA
INN SHAA ALLAH
No comments