| SIMULIZI | MAISHA YANGU 16 & 17 & 18

Share:
| SIMULIZI | MAISHA YANGU 13 & 14 & 15

Mzee habibu umri wake ulikwenda na hatimae muda wake wa kumtumikia Mkuu ulikwisha na Mkuu kuamua kumtoa sadaka. Kiukweli siku hiyo niliumia saaana maana Mzee habibu Nilikua nikimpenda saaana maana yeye Ndo aliekuwa mshauri wangu na pia ndie baba angu mlezi na ndie mtu wa peke alienileta katika ulimwengu huuu wa kichawi na kitajiri. Kiukwel katika msiba wake watu Wengi walihudhuria na Mkuu akaniamuru na kunipaisha katika nafasi ya juu ambayo alikua akimiliki Mzee habibu na kuniambia kwa hakika Mzee habibu hawez kuondoka pekee natakiwa kumfurahisha huko aliko wa damu nzito. Nilimuitikia Mkuu na kumwambia kwa hakika Siwezi kumuangusha, kwa kuwa watu walikuwa Wengi katika msiba wa Mzee habibu wakitoka kona mbali mbali maana alikua ni mtu tajiri sana na alisaidia watu Wengi. Basi ilipofika wakati wa watu wanaenda kuzika wakiwa kwenye magari niliamua kuamuru upepo mkali uliosababisha magari mawili kugongana na kusababisha vifo vya watu sita na damu nyingi saaana kumwagika barabarani. Kitendo kile kilinifanya nihisi mwili wangu Ukijawa na nguvu za ajabu na kusikia sauti ikitoa pongezi kubwa kutoka kwa Mkuu wa wakuu kutokana na kupeleka zawadi kubwa kwa ajili ya Mzee habibu. Bhasi ndani ya msiba kukazuka misiba lakini watu hawakuwaza kama ni ushirikina wala nini na kuendelea na ratiba za misiba, familia zilizopoteza ndugu zao wote niliwapa milion kumi kumi kama rambirambi na walinishukuru saana wakiniona kama mungu mtu. Siku zilisogea na umri wangu ulikwenda na hakika nilitaman kuwa na mwenza wangu wa maisha lakini niliwaza saana je akijua mie najihusisha na mambo ya kichawi atakubali kuishi na mie. Mawazo hayo yakanifanya nishindwe kabisa kuwaza tena kuhusu mahusiano lakini siku moja nikiwa supermarket nikinunua nunua baadhi ya vitu mara gafla nilipamiana na mwanamke mzuri saana tena saana. Kiukweli nilivutiwa saana na yule msichana na kuamua kumsemesha kwa maneno mengi yalioambatana na msamaha kutokana na kugongana nae bahati mbaya lakini yeye hakuonekana kuwa na time na mimi na kuniambia owk dont worry kisha akaendelea na manunuzi yake. Dada yule aliivuruga akili yangu na kunifanya nibaki nikimshangaa tu akichagua bidhaa na mie kumfwata kwa nyuma tuu taratibu na mie nikijifanya nachagua bidhaa lakini kumbe sina lolote mawazo na akili yangu ni kuendelea kumtazama mtoto mzuri. Bhasi alimaliza kuchagua mahitaji yake kisha akaelekea kwenye kulipa lakini nikamuwahi na kumwambia naomba nimlipie lakini akasema thanks kisha akalipa mwenyewe na kutoka nje. Nililipia na mie bidhaa zangu na kujaribu kutoka nje kumuwahi ni muulize angalau hata jina na kupeana mawasiliano na kujenga urafiki lakini kitendo cha kutoka nje nikakuta tiari ashapakia kwenye gari na kuanza kuondoka, nilishindwa kumzuia na kukariri namba tu za gari kisha nikaelekea kwenye gari na kurudi nyumban. Kiukweli mwanamke yule aliiteka akili yangu na kubaki nikimfikiria kila saana na kukumbuka sauti yake na jinsi alivyokuwa akitembea na kujilaumu saana kwanini nilishindwa kuomba hata namba yake sahivi angekuwa akiniliwaza kwa sauti nzuri ya kimahaba.Bhasi siku zilisogea lakini sura na sauti za mwanamke yule mrembo hazikupotea katika akili yangu na kuweka dhamira kuwa kwa vyovyote vile lazima nitampa na ndie atakuwa mwanamke wa maisha yangu. Siku zilisogea na maisha yaliendelea kwenda na mie nikawa muhudhuriaji mkubwa saana katika ile supermarket nikihisi ipo siku tu nitamuona tena mwanamke wa maisha yangu, ama kweli mungu sio athumani siku moja nikiwa natoka pale super market mara gafla namuona yule mwanamke wa maisha yangu akiwa anapokonywa vitu na vibaka kisha wakakimbia. Kiukweli katika mahusiano yangu na msichana huyu mrembo sikutaka uchawi uhusike nikihitaji hisia pekee tu ndo zizungumze kati yetu wawili. Nilipowaona wale vijana wanakimbia nilichukua gari langu na kuanza kuwafukuza kisha niliamua kutumia nguvu za kichawi kuipunguza pikipiki yao kasi na kisha nikaweza kuwafikia na kuwapush na gari pembeni wakadondoka na mie kushuka kwenye gari na kuwafwata pale chini wakiwa wameburuzika lakini hawakuumia saana kisha nikawanyang'anya pochi ile ya yule msichana mzuri kisha niwachukua na kuwafunga mikono yao na mashati yao na kurudi nao mpaka pale super market na kumkuta yule msichana akiwa analia kasimama na walinzi wa pale super market. Niliwashusha wale vijana na kumkabidhi yule msichana pochi yake na kuwaambia wamuombe msamaha yule msichana na wakiri hawatorudia tena kufanya jambo lile. Yule msichana mrembo alipokea pochi yake na kuangalia vitu vyake akakuta vipo vyote na kunishkuru saana kisha akawasamehe wale vijana na mie nikamsogelea yule msichana na kuanza kumbembeleza na kumfariji kwa kilichotokea. Msichana yule mrembo alizidi kunishukuru kila saana na kuniambia anahitaji kwenda nyumban maana wamemuharibia siku na kisha kuniachia business card yake na kuniambia tutawasiliana kama sito jali na angeniita siku moja tupate chakula cha pamoja aweze kunipa shukrani. Nilipokea kwa furaha saana business card yake na kumwambia asijal mie niko free na wala asiwaze saana kwa kilichotokea kwani ni sehemu ya purukushani za maisha na chamuhimu vitu vyake kapata basi achukulie powa. Yule msichana mrembo aliniitikia na kusema atakuwa sawa tu nisijali kisha akapanda gari na kuondoka zake, kiukweli nilihisi kama nimeondoka dhahabu chini ya muembe maana sauti na uzuri wa binti yule ulikuwa ukinichanganya haswa na kunifanya nitaman hiyo siku ya kuitwa kupata chakula ingekuwa hata muda huu maana sikutaman hata sekunde mbili awe mbali na mie

#Itaendeleaaa

No comments