| Mapishi | Aina Mbalimbali Za Upikaji Wa Ndizi

Share:


Ndizi Za Kukaanga Njegere na Nazi
MAHITAJI
Ndizi mbichi 2 – Menya kata slices
Njegere Mbichi – Mkono mmoja ( zinazo jaa katika kiganja chako)
Kitunguu maji 1 – katakata
Karoti 1 – kata vipande vikubwa vikubwa
Kitunguu swaumu punje 1 – katakata
Tui la Nazi kikombe kimoja ( lile tui la kwanza tu)
Mafuta ya Kupikia – kwa kuzikaanga ndizi
Mahanjumati masala kijiko 1 cha chai – Kama hauna hii waweza tumia spice mix yoyote uipendayo
Chumvi kiasi upendacho
JINSI YA KUPIKA
1. Kaanga ndizi ziive na kuwa na rangi kama khahawia kwa mbali. Kisha epua weka kando
2. Katika pan moja weka Kitunguu maji, kitunguu swaumu, karoti na mafuta ya kula kijiko kimoja cha mezani, vikaange kwa kwa dakika 2-3 kisha weka chumvi na masala uliyonayo kanda kidogo weka njegere koroga na weka maji kidogo kama vijiko vinne vya mezani. Funika kwa dakika 1-2
3. Sasa weka tui la nazi koroga likichanganyika weka ndizi na endelea kukoroga kwa dakika 1 ; kisha pakua katika bakuli ni tayari kwa kula


mchanyato wa Ndizi

Mahitaji:
Ndizi za kupika(ndizi bukoba) kubwa 5.Menya,kata katikati ukipenda
Viazi ulaya 4 vikubwa.kata katikati kwa urefu
Nyama kilo 1.chemsha adi iive
Nyanya 4 kubwa.sugua au saga
Nyanya ya kopo kijiko 1 cha chai
Vitunguu 2 vikubwa
Carry powder kijiko 1 cha chai
Karoti 2 kubwa.kata duara
Royco mchuzi mix,kijiko 1 cha chai
Mafuta ya kupikia,kiasi upendacho
Chumvi
[​IMG]
Njia
1.Katika sufuria weka mafuta,vitunguu ,na carry powder.Kaanga pamoja adi vitunguu viive,Ongeza nyanya ya tunda na nyanya ya kopo, kaanga adi nyanya iive.
Vitunguu viive lakini visiwe na rangi ya brauni iliyokooza
Ili kujua nyanya imeiva ,nyanya na mafuta vitatengana ndani ya sufuria.Nyanya isipoiva matokeo ya pishi hili hayatakua mazuri kama itakiwavyo.
2.Ongeza Ndizi na viazi,kaanga kwa pamoja kwa muda adi uone nyanya inashikana na viazi na ndizi.Ongeza nyama(bila mchuzi) endelea kukaanga kwa pamoja kwa dakika moja au zaidi.Ongeza mchuzi wa nyama adi ufunike mchanganyiko wa ndizi na yazidi kwa kwa inchi moja.Funika na acha vichemke kwa moto mdogo.
Kama mchuzi wa nyama ni kidogo,basi changanya na maji
Pika chakula hiki kwa moto mdogo (simmer).Moto ukiwa mkali,mchuzi utakauka kabla ya ndizi na viazi kuiva na utalazimika kuogeza maji na utakua umeharibu pishi hili.
3.Vinapoelekea kuiva,ongeza royco,chumvi na Karoti.Tingisha au zungusha sufuria ili kuchanganya ,Acha vichemke adi viive.Chakula tayari kwa kula.
Chakula hiki kikiiva kinatakiwa kubaki na mchuzi ambao ni rojo.Hivyo zingatia sana kipimo cha maji na mchuzi wa nyama unachoweka.Na hakikisha hukaushi mchuzi wote unapopika.
ENJOY MLO WAKO


Mapishi ya Mchemsho wa ndizi na nyama
Mahitaji
Ndizi mbichi 6
Nyama ya ng'ombe (nusu kilo)
Viazi mviringo 2
Kitunguu swaum
Tangawizi
Kitunguu maji
Nyanya 1 kubwa
Mafuta (vegetable oil)
Chumvi
Limao
Pilipili
Matayarisho
Chemsha nyama na limao, kitunguu swaum, tangawizi chumvi na maji kiasi mpaka nyama iive, Hakikisha unaiacha na supu kiasi kwa ajili ya kuwekea kwenye ndizi.Kisha katakata nyanya na vitunguu na uweke pembeni .Menya ndizi na viazi kisha zichemshe pamoja na vitunguu, nyanya, maji kidogo, mafuta na uhakikishe haziivi kabisa. Baada ya hapo tia nyama na supu yake, pilipili mzima na chumvi na uache uchemke mpaka ndizi na viazi viive.Na baada ya hapo mchemsho wako utakuwa tayari kwa kuliwa


MAHITAJI
Ndizi mzuzu mbichi 6 Menya na uzikate vipande vipande
Nyama ya Ng’ombe 1/4 kg
Vitunguu maji 2 Katakata
Punje 3 za kitunguu swaumu – katakata
Chill flakes ( Hiyari)
Karoti moja – katakata
Pilipili Manga – Nusu kijiko cha chai
Chumvi kiasi upendacho
Maziwa fresh 1/4 ltr
Viungo vya majani majani mf Rosemary, Oregano, Giligilani – weka kama kijiko 1 cha chai
JINSI YA KUPIKA
1. Chemsha kwanza nyama; hadi kuiva vizuri. Tunachemsha nyama kwanza maana ndizi huiva haraka
2. Kisha weka ndizi na hivyo vingine isipokuwa maziwa. Chemsha ziive kabisa
3. Kisha weka maziwa koroga huku inachemka kwa dakika 5 baada ya hapo epua na ni tayari kwa kula

No comments