Wasifu wa IGP SIMON NYAKORO SIRRO

Share:

IGP mpya wa jeshi la polisi aliyeteuliwa usiku wa 28.05.2017 na rais na hatimae 29.05.2017 akaapishwa ikulu na kuchukua kiti hicho rasmi.

IGP Simon Nyakoro Sirro kabla ya kuteuliwa kuwa IGP alikuwa ni kambishna wa police kanda maalum ya dar es salaam nafasi hiyo akiipokea kutoka kwa Suleiman Kova mnamo 15/02/2016 ambaye alistaafu baada ya kushika nafasi hiyo tokea mwaka 2008 nae alipokea kwa Kamanda ALFRED TIBAIGANA





IGP Simon Nyakoro Sirro aliwahi kuwa mkuu wa upelelezi katika kituo cha buguruni , tarafa ya magomeni, mkuu wa upelelezi msaidizi mkoa wa Tabora, na pia mwaka 2002 alikuwa mkuu wa upelelezi msaidizi wa Dar es salaam.

IGP Simon Nyakoro Sirro kabla ya kuwa kamishna kanda maalum dar es salaam alikuwa mkuu wa operation wa jeshi la polisi na aliwahi dhibiti wahamiaji wengi mwaka 2012.

Pia IGP Simon Nyakoro Sirro pia amewahi kuwa kamanda katika mikoa mbalimbali kama Tanga, Mwanza na Shinyanga

IGP Simon Nyakoro Siro anakuwa IGP wa 10 sasa katika jeshi la polisi tokea wa Elangwa Shahidi 1964 mpaka kwa Ernest Mangu aliemkabizi 2017.


No comments