NUKUU 10 ZA BABA WA TAIFA MWALIMU JK.NYERERE
1. " Kutokana na umri mkubwa wa chama chetu cha CCM, watu wengi wenye kasoro wamejiingiza kwenye chama hiki. Sasa kimekuwa kama dodoki ambalo linabeba vitu visafi na vichafu. Sasa tumekuwa na watu wa ajabu sana ndani ya chama chetu".
2."Nchi yetu inaongozwa na sheria. Hatuwezi kuchagua kiongozi asiyeheshimu sheria akawa anaongoza nchi kwa kushauriwa na mkewe, maana hamjui kesho akiamka atamshauri nini".
3." Watanzania wakiyakosa maendeleo ndani ya CCM, watayatafuta nje ya CCM".
4." Inawezekana tatizo la paka kwa panya lingekwisha kwa paka kufungwa kengere shingoni; tabu ni kumpata panya wa kufanya kazi hiyo. Na panya watakuwa wajinga sana kwa kudhani paka watajifunga au kufungana kengere".
5 " Tunataka kuona vijana jeuri katika Taifa hili na wenye kujiamini na sio waoga akina " ndiyo bwana mkubwa". Tunataka kuona vijana wenye ujasiri wa kuhoji na kupiga vita mifumo ya kidhalimu isiyoshabihiana na matakwa na matarajio ya jamii ya kitanzania. Tunataka vijana waasi mifumo kandamizi, ubwana na ufisadi katika Taifa".
6. " Udikteta ni serikali ya mtu mmoja au kikundi cha watu wachache ambao wao ndio huwa sheria, anayepinga watakayo huoneshwa cha mtema kuni".
7." Makosa yetu mengine hutokana na woga: woga wa kujizuia kumlaumu mkubwa japo tunajua kakosea au woga wa kumtetea mdogo anaelaumiwa na mkubwa japo tunajua hana kosa".
8."Amini nawaambieni enyi waswahili wachache mnaotawala, mnaamini kweli mtawaongoza watanzania kwa lazma wakati wamepoteza matumaini na mtegemee watakaa kwa amani na utulivu? Amani ni zao la matumaini. Pindi matumaini yanapotoweka kutakuwa na vurugu katika jamii. Nitashangaa kama hawa watanzania watakataa kuasi. Kwanini wasiasi? Wananchi wanapopoteza matumaini unajenga volcano. Volcano hii italipuka siku moja, labda kama watu hawa ni wajinga. Watanzania watakuwa ni wajinga na mataahira kama watakubali kuendelea kukandamizwa na watu wachache katika nchi yao wenyewe".
9." Nawaambieni na msikilize kwa makini: UTII ukizidi sana unakuwa WOGA. Mara zote utii huzaa unafiki na kujipendekeza. Sasa nyinyi watumishi wa umma kwa wingi wenu kama mmeshindwa kupiga kura kuondoa viongozi dhalimu, bora mfe tu".
10. " Siku inakuja ambapo watu watachagua kifo kuliko fedheha na nawahurumia Watanzania watakaoiona siku hiyo! Na ole wao watakaoifanya siku hiyo isiepukike. Natumaini na kusali kuwa siku hiyo kamwe isifike".
No comments