|MAPISHI | Mchicha (Swiss Chard) Na Bamia

Share:

  
Vipimo  
Majani ya Mchicha (Swiss Chard) - 4  - 5 
Bamia - 150 - 250g 
Chumvi - 1 kijiko cha chai 
Mafuta ya zaituni - ½  kikombe 
Maji - 1 gilasi          
Kitunguu maji kilokatwakatwa - 1  
Namna Ya Kutayraisha Na Kupika  

  1. Katakata sehemu ya juu ya majani ubakishe majani pekee. 
  2. Osha majani kisha katakata kama mchicha wa kawaida . 
  3. Tia mboga katika sufuria, maji na chumvi chemsha kwa dakika 25 hivi. 
  4. Osha bamia  uweke tayari ukiwa umezikata vikonyo vyake. 
  5. Mboga ikishachemka kurudia chini mimina bamia, kitunguu, mafuta . Acha ichemke mpaka bamia ziwive ikiwa tayari. 

No comments